Skip to content

Kuunda mfumo wa kiuhasibu kwenye CAMS

Tumetumia muda wa kutosha pamoja na SACCOs wakijaribu  mifumo yetu na kuhakikisha kwamba vipengele kwenye CAMS viko 100% na vinawiana na kile kinachohitajika. Maoni mawili makuu ambayo yamekua yakijirudia kwetu ni Mfumo wa kihasibu na shughuli za dawati la mbele kwenye saccos (teller functionality). Ili kutengeneza vipengele hivi,tumesogeza uzinduzi mbele na kuelekeza juhudi zetu kwenye muelekeo huo ambao tumejifunza kutoka kwa wateja wetu.

Pia tunazidi kujenga timu yetu nchini Tanzania kwenye mawasiliano, uhasibu na uwajibikaji wa kisheria.

Kwa kumalizia, tunaelewa kuwa mambo haya tunayojifunza tukiwa na wateja wetu ni muhimu sana na tungependa kukushukuru sana kwa kutuongoza.