Skip to content

Safari ya Wakandi pamoja na Ushirika na SCCULT nchini Tanzania

Wakandi ilialikwa na SCCULT (The Savings and Credit Cooperative Union League of Tanzania ) kuwa sehemu ya mafunzo maalum Tanzania bara. Mafunzo haya yalifanyika kwa kushirikiana na Ushirika (Tanzania Cooperative Development Commission) kuhusiana na  maandalizi ya ripoti za kiutendaji na usimamizi wa SACCOs zilizo na leseni Tanzania.

Mafunzo hayo yaliundwa na SCCULT kwaajili ya uongozi wa SACCOs na viongozi ambao wanahusika kwenye maandalizi, ujazaji na uwasilishaji wa ripoti za mwezi za kiutendaji kwenye SACCOs zenye leseni daraja B  na ripoti za robo mwaka za  kiutendaji kwa SACCOs zenye leseni daraja A. 

Rahma Amani kutoka  Wakandi Tanzania aliungana nao kwenye safari, kusambaza elimu juu ya ripoti za Ushirika na kuzielezea SACCOs umuhimu wa kukaguliwa uwajibikaji kwenye masuala ya kisheria.

Ilikua ni fursa nzuri sana ya kujifunza kwa Rahma kuwa sehemu ya mafunzo hayo. Anasema “SACCOs wanakumbana na changamoto kwenye kujenga ushindani wa kihasibu. Uwepo wa CAMS kama suluhisho unaweza kuwa hatua muhimu kwa SACCOs kwenye kufanikisha uwajibikaji kwenye masuala ya kisheria” 

Hassan Mnyone, Mkurugenzi mkuu wa SCCULT anaamini kwenye mfumo wetu na manufaa unayotoa. Hassan anasema, “Kupitia mfumo wa CAMS, Wakandi itawezesha upatikanaji wa taarifa muhimu zinazohitajika, kama taarifa za shughuli mbalimbali za vyama, ikiwemo hizi ripoti za ushirika (MSP) ambazo ndio zinatolewa mafunzo.”

Tunatarajia fursa nyingi zaid kama hizi mbeleni kushirikiana na kufanya kazi pamoja kuzisaidia SACCOs kufanikisha uwajibikaji bora wa kisheria na ukuaji mkubwa.