Skip to content
feature-image

"Sasa tunatunza kumbukumbu kiufanisi na tuna uwazi kwenye SACCOs yetu"

Hitaji la huduma ya mikopo kwa watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoani Tabora lilikuwa ni muhimu. Hitaji hilo lilikuja na changamoto ya riba kubwa na masharti ya kuomba mikopo kwenye mabenki. 

Katika kutafuta suluhu, hapo ndipo TUWASA SACCOs ikazaliwa mwezi November mwaka 2011 ikiwa ni SACCOs ya waajiriwa iliyoanza na wanachama 41 kwa lengo la kukopeshana na kuweka akiba ili kuboresha maisha. 

Katika safari ya TUWASA SACCOs, kuliibuka changamoto nyingine kubwa ambayo ni utunzaji wa taarifa za kifedha na uendeshaji wa umoja huo kupelekea kushindwa kudhibiti mikopo na marejesho ya wanachama kupitia mishahara yao mwisho wa mwezi kwa ufanisi hadi pale mfumo wa  TUWASA ilipokutana na Wakandi mwaka 2022.

“Wakati tunatumia excel ilikuwa ni rahisi mtu yeyote kufikia na kubadilisha taarifa,lakini pia taarifa huweza kupotea, lakini kutumia mfumo huu wa CAMS, taarifa zinakuwa salama” Mhasibu, TUWASA SACCOs. Saimon Kasya,  

TUWASA ambayo sasa inatumia mfumo wa Wakandi CAMS imefurahishwa na ufanisi, urahisi na udhibiti wanaoupata kwenye mfumo huo ikiwemo kupata ripoti za SACCOs kiotomatiki, pia kupunguza kazi kwa watendaji ambao mara nyingi huwa katika majukumu yao ya kiofisi kama waajiriwa wa mamlaka ya maji safi mkoani Tabora.

“Tunafurahi sana kuwa na Wakandi, mfumo umeturahisishia mambo mengi, la kwanza, kutunza kumbukumbu la pili kuwa na uwazi, wanachama wanaamini kile kitu tunachokifanya kwenye chama chetu” Evans Binya, Mwenyekiti, TUWASA SACCOs. 

Mwenyekiti wa TUWASA SACCOs, Ndugu Evans Binya akielezea historia ya TUWASA na namna iliyonufaika na mfumo wa Wakandi CAMS.

Wakandi iliwakaribisha wawakilishi wa TUWASA SACCOs, mwenyekiti, Evans Binya na mhasibu ndugu Saimon Kasya kwenye ofisi za Wakandi jijini Dar es Salaam, ambapo walipata mafunzo ya kina kuhusu mfumo wa CAMS kutoka kwa wataalamu kwa Wakandi. 

Boaz and TUWASA certificate picture 3Meneja wa Wakandi Tanzania, Bw. Daudi Boaz akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa TUWASA Bw. Evans Binya na Mhasibu wa TUWASA Bw.Saimon Kasya kama utambuzi wa kupokea mafunzo ya mfumo wa Wakandi CAMS, yaliyofanyika ofisi za Wakandi, jijini Dar es Salaam.

Mfumo wa Wakandi CAMS umekuwa ukisaidia vyama vya ushirikia nchini Tanzania na nchi za jirani kama Kenya na Uganda kusimamia taarifa za kifedha kidigitali.

Jaribu Demo ya CAMS