Skip to content

Wakandi CAMS – Mfumo wa uhasibu wa kuingia mara mbili uliojumuishwa kikamilifu 

Wakandi’s Credit Association Management System (CAMS) unatoa mfumo kamili wa kihasibu pamoja na Microfinance. Kama kifaa cha kihasibu, inapunguzia saccos nguvu ya kusimamia kazi nyingi za karatasi, vile vile ina vipengele vingi na manufaa kuliko mifumo ya kihasibu iliyopo sasa. CAMS inaleta mfumo wa kihasibu wenye maingizo ya pande mbili inayosaidia na kusimamia miamala yote ya SACCOs lakini pia inashughulikia miamala iliyofanya na mwanachama mmoja mmoja. 
 
Chini ya mfumo wa kihasibu wa CAMS, SACCOs inaweza kusimamia miamala kama: 

  • Mapato na matumizi  
  • Mapato ya biashara   
  • Matumizi  
  • Akaunti za akiba  
  • Akaunti za hisa  
  • Utoaji mikopo na malipo ya mkopo   
  • Taarifa za Kodi    

Kwa kuongezea, mfumo wa kihasibu wa CAMS ni wa ufasaha wa hali ya juu na unaweza kusimamiwa na wafanyakazi wachache kama keshia. Mfumo huu  

  • Unatoa Chati za akaunti,   
  • Unaweka rekodi ya mali zote,   
  • Unachakata ripoti zikiwemo urari, mizania, mapato na matumizi, leja, kitabu cha keshi, kitabu cha jono nk.   
  • Unasapoti maingizo ya aina zote (Jono, Contra, Malipo na risiti)  

Umuhimu wa mfumo wa kihasibu kwenye CAMS  

Mfumo wa kuhifadhi taarifa ni muhimu kwa kila SACCOs. Zifuatazo ni baadhi ya umuhimu wa kutumia mfumo wa kihasibu: 

Picha kamili ya kihasibu  

Ni muhimu kila SACCOs itunze taarifa zake.Hii ni kwasababu uhifadhi wa taarifa kwa namna ya maingizo ya pande mbili  inasaidia kuandaa ripoti muhimu za kihasibu kama  urari, mizania pamoja na kitabu cha jono. Mfumo wa kihasibu wa CAMS pia utakupa taarifa kamili kuhusiana na miamala kulinganisha na mifumo wa maingizo ya upande mmoja (single-entry system) kwasababu kila muamala una chanzo chake na kikomo chake.    

Maamuzi sahihi ya kifedha  

SACCOs inaweza kusimamia shughuli zao kwa kuweka rekodi ya akaunti zao kwa kushirikiana na mfumo wa kihasibu wa maingizo ya pande mbili. Kwa kuongezea inaonesha ni kwa kiasi gani SACCOs imefanikiwa na imekua imara kifedha kwenye kusaidia kufanya maamuzi ya kifedha.  
SACCOs inaweza kulinganisha akaunti mbalimbali kupitia taarifa zilizohifadhiwa kwenye mfumo wa kihasibu. Taarifa mbalimbali za miaka iliyopita pamoja na za miaka ya sasa zinaweza kulinganishwa na tofauti zitakazogundulika zinaweza kurekebishwa.   

Inaondoa makosa ya kuhifadhi taarifa  

Kwenye mfumo wa kihasibu wa CAMS, mali,madeni pamoja na mtaji inabidi ziwe sawa.Kama sio sawa, maingizo ya kwenye mfumo sio sahihi, ambayo inamaanisha itakua rahisi kugundua makosa yamefanyika wapi na kusahihisha kwenye chanzo. 
Maingizo ya pande mbili kwenye uhasibu unahakikisha mizania pamoja na vitabu vya kihasibu viko sahihi. Kuwa sahihi pia inasaidia keshia wa SACCOs kupunguza makosa. 

Inapendekezwa na benki na vyombo vya udhibiti    

Mfumo wa kihasibu wa CAMS una ufanisi na uwazi.Inafanya iwe rahisi kwa SACCOs kupata fedha na kuwa sehemu ya mjumuisho wa fedha. Njia ya maingizo ya pande mbili kwenye uhasibu unatengeneza ripoti zinazoipa benki pamoja na wawekezaji maono ya usahihi kuhusiana na fedha kwenye SACCOs  
Hii njia ya kuhifadhi taarifa inapendekezwa na benki pamoja na vyombo vya udhibiti.   

Inajenga historia ya ukopaji kwa wanachama wa SACCOs  

Mfumo wa kihasibu wa CAMS utawezesha SACCOs kujenga historia ya ukopaji kwa wanachama wao. Moja kati ya sababu kuu kwanini  wanachama wa SACCOs hawana akaunti za benki na sio sehemu ya mjumuisho wa kifedha ni uwezo wao wa kukopesheka (credit ratings) haupo. Kwa kutumia mfumo wa kihasibu wa CAMS, itakua rahisi kufuatilia miamala ya wanachama kwenye mikopo, hisa na akiba  hivyo kutengeneza historia ya ukopaji.   
Mfano mzuri wa mfumo huu ni madereva wa bodaboda ambazo hawana uwezo wa kuchukua mkopo au mkopo unagaiwa kwao kwa riba kubwa sawa na gharama za kutengeneza pikipiki hizo au kununua mpya. 
Kama sehemu ya SACCOs, madereva wa bodaboda wataweza kujitengenezea ripoti za kukopesheka nakuomba mikopo benki.