Tunahamasa kubwa kukushirikisha habari njema. Tunafanyia kazi kipande cha Uhasibu kwenye CAMS – kipengele cha upande wa watendaji ili kuwezesha kutengeneza ripoti za kihasibu na kifedha. Itakua ni kipengele kwenye eneo la menyu ili uweze kutengeneza na kusimamia kiurahisi ripoti mbalimbali kama mizania, urari na kusimamia akaunti kiujumla.
Uhasibu kwenye CAMS itatolewa ili kusaidia uundaji wa ripoti za kihasibu kiautomatiki kwaajili ya watendaji wa SACCOs. Itarekodi miamala ya kila siku ili kuhakikisha ripoti zinatoka kwa usahihi. Kwa kutumia ripoti hizi, uongozi wa SACCOs unaweza kupata mwanga kwenye mapato yao,mikopo yao, matumizi yao pamoja na nafasi ya kifedha ya chama kiujumla. Mfumo wa kihasibu utatoa manufaa yafuatayo kwa SACCOs-
- Muda wa kusasisha akaunti: Muda unaotumika kutally na kusasisha unaweza kupunguzwa kutoka wastani wa masaa 24 mpaka dakika moja.
- Upunguzaji wa gharama za kujiendesha: Upunguzaji wa shughuli za karatasi na muda wa watu kufanya kazi, utafanya mchakato mzima wa kuomba mkopo kuwa usio chosha na kwa gharama nafuu kwa SACCOs.
- Taarifa zenye usahihi zaidi: Utunzaji wa taarifa kidigitali unaondoa makosa yatokanayo na maingizo yasiyo kidigitali na makadirio. Hivyo kupunguza ubatilishaji wa taarifa na migogoro.
- Ufanyaji maamuzi na udhibiti unaotegemea taarifa: Mfumo wa kihasibu kidigitali utasaidia kuwepo na usawa kwenye maamuzi ya mkopo na usimamizi, kwa kufanya mchakato kuwa kidigitali na kuepuka upendeleo.
- Uwiano wa kisheria: Mfumo wa kihasibu uliowezeshwa kiteknolojia unahakikisha uwiano wa kisheria na tume ya Ushirika na Benki kuu ya Tanzania kwa SACCOs za daraja B.
- Utengenezaji wa ripoti za Ushirika (MSP reports): Mfumo wa kihasibu kidigitali utatengeneza ripoti za usahihi zaidi za ushirika (MSP reports) na kusaidia kutii kanuni nchini Tanzania.
Tutazidi kukufahamisha kadri tunavyofanyia kazi kipengele hiki kipya. Kaa tayari kusimamia kwa ubora shughuli za kifedha kwenye SACCOs yako.
We are excited to share some good news with you. We are working on CAMS Accounting – a double entry accounting feature in the CAMS Admin portal to create different types of accounting and financial reports. It will be baked into the menu section of the app so that you can easily create and manage reports like balance sheets, trial balance, and maintain general accounts.
CAMS Accounting will be offered to automate creating accounting reports for SACCO admins. It will record day-to-day transactions to create accurate reports. Using these reports, the SACCO management can gain insights into their dividends, loans, expenses and overall financial position. The accounting system will offer the below-mentioned advantages to SACCOs-
- Account updation time: The time taken to tally and update records can be reduced from an average of 24 hours to under one minute.
- Decreased operational costs: The reduced paperwork and staff time will make the loan process less tedious and expensive for the SACCOs.
- More accurate data: Digital recordkeeping eliminates errors due to manual entry and estimations, thereby reducing data manipulation and disputes.
- Data-based decision-making and controls: The digital accounting system will enable fairness and uniformity in credit decisions and administration by automating processes and avoiding bias.
- Compliance-friendly: The tech-empowered accounting system ensures statutory compliance with TCDC and BoT for category B SACCOs.
- Generation of MSP reports: The digital accounting system will generate more accurate MSP reports and help to meet the regulations in Tanzania.
We will keep you updated as we work on this new feature. Get ready to enhance the financial operations of your SACCOs.