Taasisi ndogo za fedha na Vyama vya Ushirika vimeendelea kuwa mkombozi wa jamii. Kupitia SACCOS na Microfinance, idadi kubwa ya wanajamii imekuwa ikunufaika kupitia mikopo inayotolewa ili kuboresha maisha, kama lilivyo kusudio la kuundwa kwa vyama hivyo.
Katika kuendelea kutambua mchango wa vyama hivi, Wakandi Tanzania tunayo furaha kuzindua bidhaa mpya ya Bima ya Ulinzi wa Mkopo, baada ya kupewa leseni ya kuendesha shughuli za Bima Kidigitali chini ya mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania, TIRA.
Uzinduzi rasmi wa bidhaa ya Bima ya Mkopo Kidigitali
Kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Sanlam, Wakandi ilizindua rasmi bidhaa ya Bima ya Ulinzi wa Mkopo kidigitali, Agosti 14 katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam, mbele ya Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo Saqware akiwa kama mgeni ramsi wa tukio hilo muhimu.
Akielezea bidhaa hii ya Bima ya Ulinzi wa Mkopo ya Wakandi na Sanlam, mkuu wa kitengo cha Bima, Wakandi, Bw. Masoud Mndeme aligusia namna vyama ushirika na taasisi ndogo za fedha zitakavyojiepusha na hatari za kuingia hasara kwa upande mtoa mikopo na pia upande wa mkopaji.
Mkuu wa kitengo cha Bima kutoka Wakandi, Bw. Masoud Mndeme.
“Inapotokea bahati mbaya mkopaji amefariki na ana deni la mkopo kwenye chama, Bima hii italipa deni lote. Hii itamuweka mkopeshaji kuwa na ulinzi wa mikopo anayotoa kuepusha hatari za kupata hasara. Kama hiyo haitoshi mwanachama anapofariki na deni, familia yake inakuwa na amani na utulivu wa akili kwa sababu, haitorithi madeni” Masoud Mndeme, Wakandi Tanzania.
Mgeni rasmi wa tukio hili muhimu, Dkt. Baghayo Saqware, katika hotuba yake nzuri, Dkt. Saqware alizindua rasmi na bidhaa ya Bima ya ulinzi wa mkopo ya Wakandi, iliyoandikwa na kampuni ya Sanlam.
“Ni matumaini yangu kuwa bidhaa hii itaboresha usalama wa kifedha na hatimaye kuongeza mchango katika ukuaji wa sekta ya Bima, nawapongeza sana Wakandi na Sanlam kwa bidhaa hii muhimu sana kwa ajili ya kuendeleza vyama vya ushirika. Sasa natangaza bidhaa ya Bima ya Mkopo kidigitali ya Wakandi, kwa kushirikana na Sanlam, imezinduliwa rasmi” Dkt. Baghayo Sakware, Kamishna wa Bima, TIRA.
Mgeni ramsi, Dkt. Baghayo Sakware, Kamishna wa Bima, TIRA akitoa hotuba.
Ushirikiano baina ya Wakandi na Sanlam
Sanlam na Wakandi tumeingia makubaliano ya kibiashara yanayoleta huduma bora ya Bima ya Mkopo Kidigitali ambapo kupitia mfumo wa Wakandi CAMS, unaosaidia SACCOS na Microfinance kusimamia na kuendesha shughuli za fedha kidigitali, sasa taasisi hizi zinaweza kukatia Bima mikopo inayotolewa wateja wao.
“Sisi na Wakandi tuna lengo moja linalofanana, tunataka kutoa ulinzi kwa asasi ndogo ndogo kama SACCOS kuweza kujikimu kiuchumi. Lakini ili SACCOS au taasisi ndogo ya fedha iweze kuendelea na kukopesha watu wake wenye uhitajii kujikimu kiuchumi, ni lazima ule mtaji wa SACCOS au Microfiance ulindwe, lakini mkopaji pia alindwe ili kukitokea tatizo familia yake ibaki salama” amesema hayo Bw. Julius Magabe, Afisa Mtendaji Mkuu, Sanlam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Bw. Julius Magabe
Kwa upande wa Wakandi, Mkurugenzi Mkaazi wa kampuni Bw. Daudi Boazi alisema " Wakandi tumeona Sanlam ndio kampuni inayoendana na maono yetu ya kuleta maendeleo kwa wanaushirika, tunaamini ubora wa huduma zao na ukubwa wao vinaendana na picha kubwa tuliyonayo Wakandi. Huduma hii ya Bima ya Ulinzi wa Mkopo ya Wakandi, iliyoandikwa na Sanlam itanufaisha taasisi ndogo za fedha na wanachama wake".
Baada ya uzinduzi huu, nini kinafuatia?
Baada ya Kamishna wa Bima kuzindua rasmi bidhaa ya Bima ya Mkopo kidigitali ya kampuni ya Wakandi kwa kushirikiana na Sanlam, Vyama vya Ushirika na taasisi ndogo za fedha sasa wanaweza kujiunga na Bima hii kujihakikishia usalama wa mikopo pamoja na mustakabali wa wanachama. Rasmi kabisa bidhaa hii ipo tayari kuanza kutumika nchini Tanzania.
Jiongeze na Bima ya Mkopo Kidigitali leo.